Viongozi wa klabu ya Yanga wameendelea kuonyesha jeuri kwa kutangaza kuingia sokoni mara tu baada ya dirisha dogo litakapofunguliwa disemba 16. Mbali na wachezaji wake
kadhaa wa kimataifa kuandika barua za kuachana na Yanga, uongozi wa klabu hiyo umewataka wanachama na mashabiki wake kutokuwa na wasiwasi.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Hassan Bumbuli, amewaambia wanayanga wote kutokuwa na wasiwasi sababu wamejiandaa kufanya usajili wa maana dirisha dogo.
Usajili ambao Yanga wanalenga zaidi kuufanya ni nafasi ya ushambuliaji ambayo imeonekana kuwa na mapungufu zaidi.
Ameeleza wamedhamiria kufanya usajili wa maana kutokana na mwenendo wa timu namna ulivyo kiasi cha kwamba imepelekea kisiwe na matokeo mazuri katika siku za hivi karibuni.
"Nawaomba wanayanga wasiwe na wasiwasi.Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya kufanya usajili wa maana kunako dirisha dogo.Tunalenga zaidi kuzingatia eneo la ushambuliaji ambalo linaonekakana kuwa na mapungufu mengi."
1 Comments
Habari za wakati huu
ReplyDelete