Klabu ya Yanga imeanza kupigwa chini na baadhi ya wachezaji wa kigeni wa Klabu hiyo kufuatia kushindwa kuwalipa mishahara yao.chanzo makini kimenukuu
"Sadney Urikhob ameshaondoka Yanga SC kufuatia makubaliano binafsi na uongozi wa klabu yetu, Sadney alikuwa na mkataba na Yanga SC hadi september 05, 2021! Mnamibia huyo amelazimika kuondoka Yanga kufuatia kutolipwa mishahara na bonus kama mkataba wake unavyoainisha , maamuzi kama hayo pia yamefikiwa na Lamine Moro ambaye yupo kwao Ghana kwa sasa!
Uongozi umekiri kutowalipa mishahara wachezaji kwa muda wa miezi miwili mpaka sasa na kuahidi kutolea ufafanuzi siku ya jumanne lakini wanapambana kuhakikisha kulipa mishahara ya miezi mitatu ndani ya siku saba zijazo.
0 Comments