BETI NASI UTAJIRIKE

WACHEZAJI KIKOSI CHA TATU YANGA WAANZA KUTOA VIPIGO KIGOMA

Klabu ya Yanga ipo mkoani Kigoma kwa mechii za kirafiki ikijiandaa kurejea Ligi kuu bara kwa kishindo. Ynaga watakuwa na kibarua kigumu mwezi Januari dhidi ya  wapinzani wao


wa jadi Simba mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam tarehe 04 Januari. IKiwa mkoani kigoma klabu hiyo itacheza mechi kadhaa na kuhamia mikoa mingine kwa mechi hizo. 

Hapo jana klabu hiyo ilicheza mchezo wake wa kwanza wa  kirafiki dhidi ya Mwamgongo fc na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Mchezo huo uliigwa dimba la Lake Tanganyika  Mjini Kigoma.

Mwamgongo FC walikuwa wakwanza kupata bao kupitia Abdulazak Boban lakini Adam Stanley na Mapinduzi Balama wakachomoa na kuongeza bao la ushindi. Klabu hiyo itatumia wachezaji wengi wa kikosi cha pili kwani wachezaji wa kikosi cha kwanza wapo kwenye michuano ya CECAFA 2019 nchini Uganda huku wengine wakiwa mapumzikoni

Siku ya Jumapili klabu hiyo itacheza mchezo wa pili wa kirafiki dhidi ya Klabu ya Mbao inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara pamoja na Yanga .


Post a Comment

0 Comments