BETI NASI UTAJIRIKE

UJUMBE WA MESSI BAADA YA KUSHINDA BALLON D OR

Mshambliaji wa Barcelona na Argentina ameweka rekodi mpya barani duniani baada ya kushinda tuzo za Ballon D'Or mwaka 2019 ikiwa ni mara ya Sita ndani ya miaka 12 Lionel Messi ameonekana kufurahishwa na ushindi wa tuzo hizo zilizotolewa jijini Paris Ufarasa akiwamwaga beki wa Liverpool Van Dijk na Cristiano Ronaldo wa Juventus.  Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa upigwaji wa kura kutoka kwa makocha ,Makapteni na waandishi wa habari tulishuhudia Lionel Messi akipata kura nyingi zaidi ya wapinzani wake.

Lionel Messi amenukuliwa akisema " Shukrani za dhati ziliendee shirikisho la soka Ufaransa na waandishi wa habari walioniigia kura. Nisingefanikiwa kushinda tuzo hii bila wachezaji wenzangu wa Barcelona na timu ya taifa Argentina , hivyo tuzo hiii ni yao pia. Tuzo hii pia inamilikiwa na familia yangu kwani wamekuwa wakinipa sapoti kila siku"

Lionel Messi ameendelea kuweka rekodi mpya kila siku kwani majuzo tu amefanikiwa kuweka rekodi ya kucheza michezo 700 pia akiweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee aliyezifunga timu 34 tofauti ligi ya mabingwa ulaya akifunga jumla ya mabao 113.

Post a Comment

0 Comments