BETI NASI UTAJIRIKE

UCHAMBUZI:SABABU ZA ARSENAL KUFUNGWA ,MAKOCHA WAO HAWAHUSIKI

Klabu ya Arsenal imeendelea kuwa na wakati mgumu msimu muu baada ya kulazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya Standard Liege kwenye michuano ya Europa league hatua ya 


makundi. Mwishoni mwa mwezi Novemba klabu hiyo ilimfuta kazi mkufunzi wake Unai Emery kwa madai ya kushindwa kupata matokeo mazuri klabuni hapo hasa ligi kuu Uingereza. Uongozi wa Klabu hiyo uliamua kumkabidhi timu hiyo mchezaji wake wa zamani na kumkabidhi Freddie_Ljungberg. 

Kocha huyo ameiongoza Arsenal kwa mechi nne na amepata sare mbili dhidi ya Standard Liege na Norwich zzote akipata sare za mabao 2-2 ,Akifungwa na  Brighton mabao 2-1 na kushinda mabao 3-1 dhidi ya Westham.

Haya ndiyo matatizo yanayopelekea  Arsenal kufugwa

Eneo la Ulinzi

Eneo la ulizi la klabu ya Arsenal limeonekana kuwa dhaifu msimu huu, klabu hiyo imeruhusu mabao 24 kwenye mechi 15 ilizocheza. Hapa wanatakiwa kusajili mabeki wa pembeni kwani mipira mingi iliyozaa magoli imetokea pembeni

Eneo la Kiungo

Matumizi ya Torreira na Grant Xhaka kwa wakati mmoja binafsi naona si sahihi . Hawa ni viungo wachezeshaji na kama utawatumia viungo hawa kwa pamoja basi ni lazima ucheze 4-3-3 ikiwa na maana uwe na kiungo mkabaji , mwenye nguvu halafu Torreira na Xhaka wacheze kama viungo washambuliaji.

Eneo la Ushambuliaji

Uwepo wa Lacazzete na Aubemayang umechangia upatikanaji wa magoli 24 kwenye mechi 15 za ligi kuu. Kombinesheni hiyo imeendelea kufanya vizuri kwenye Europa League kwa kufanikisha mabao 14.

Dirisha dogo linapofunguliwa klabu hiyo italazimika kusajili wachezaji wenye viwango vya juu pasipo kuzingatia gharama. Isipofanya hivyo basi itakuwa na wakati mgumu mno mpaka mwisho wa msimu na kunauwezekano kutokuwemo top 6

Post a Comment

0 Comments