BETI NASI UTAJIRIKE

TIMUA TIMUA INAENDELEA MSIMBAZI, MWINGINE TENA KUONDOLEWA

Baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa Simba Patrick Aussems kuondolewa klabuni hapo timua timua haijaishia hapo kwani kocha msaidizi  wa timu hiyo Denis Kitambi ameanza 
kutafutiwa mlango wa kutokea. Taarifa zilizopo hivi sasa ni kuhusiana na Kocha Msaidizi wa Simba,Denis Kitamb  anaweza kuondolewa ndani ya kikosi cha kwanza.

Habari za ndani zinasema Kitambi ataondolewa ili kupelekwa katika kikosi cha vijana, Simba B na nafasi yake inaelezwa Suleiman Matola anaweza kuchukua nafasi yake.

Kitambi alichukua nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anashikiria nafasi hiyo, Masoud Djuma kutoka Burundi kushindwa kuelewana na aliyekuwa Kocha Mkuu wa wakati huo, Pierre Lechantre.

Simba hivi sasa ipo katika mchakato wa kusaka Kocha Mkuu ambaye atachukua nafasi ya Patrick Aussems ambaye ameondolewa ndani ya klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments