BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO ALHAMISI TAREHE 12-5-2019

Manchester United wanaweza kumsajili kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate endapo watamtimua Ole Gunnar Solskjaer mwishoni mwa msimu. (Sun)

Kocha msaidizi wa United Mike Phelan amesema klabu hiyo bado inataka kusajili wachezaji nyota. (Evening Standard)
Chelsea wapo tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (Goal)
Chelsea itapata majibu hii leo endapo marufuku waliopigwa ya kufanya usajili (kwa madirisha mawili) inayotarajiwa kuisha mwezi Februari kama itaondoshwa na kuruhusiwa kuingia sokoni mwezi Januari. (Daily Telegraph)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane bado anataka kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Marca)
Manchester City wanaamini kuwa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 24, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo. (Metro)
Liverpool na Arsenal wameungana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Ujerumani Karim Adeyemi, 17 kutoka klabu ya RB Salzburg. (Sport via Mirror)
Everton wanajiandaa kumpa mkataba wa muda mrefu kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Lucas Digne, 26. (Mail)
Atletico wamekubali kumsajili kiungo machachari kutoka klabu ya Athletico Paranaense ya Brazili Bruno Guimaraes, 21, kwa dau la pauni 25.4m. (UOL, in Portuguese)
Tottenham wanapanga kumsajili beki wa kati wa klabu ya Norwich Ben Godfrey, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 25. (Football Insider)
Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni "uozo" japo "haiwezekani kurudi nyuma". (Mirror)
Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal - in Spanish)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)

Post a Comment

0 Comments