BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI TAREHE 7-12-2019

Real Madrid iko tayari kuwaachilia mshambuliaji wa Colombia James Rodriguez, 28, na winga wa Wales Gareth Bale, 30, kama sehemu ya makubaliano ya kumpata kiungo wa 

kati wa Manchester United na mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba, 26. (Eldesmarque via Sunday Express)
Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc anasema mshambuliaji wa England Jadon Sancho,19, hataondoka klabu hiyo mwezi Januari, licha ya tetesi zinayomhusisha na Manchester United. (Manchester Evening News)
Naibu mkufunzi wa Manchester City Mikel Arteta atalazimika kupitia mchakato mrefu wa mahojiano ikiwa anataka kuwa meneja wa kudumu wa Arsenal. (Sunday Telegraph)

Mikel Arteta alianza kazi ya ukufunzi Manchester City mwaka 2016Haki miliki ya picha

Manchester City hawawezi kumsaini Jadon Sancho kutokana na kipengele walichoafikiana kama sehemu mkataba uliowawezesha kumuuza kwa klabu hiyo ya Ujerumani.Lakini mbaingwa hao wa ligi ya Primia hawatakubali mpango wa kulipa ofa yoyote ya kumpata tena winga huyo. (Sunday Mirror)
Mkufunzi wa Barcelona Ernesto Valverde amedokeza kuwa kiungo wa kati Arturo Vidal huenda akajiunga na Manchester United. (Sunday Mirror)
Real Madrid lazima ikusanye £84m katika mauzo ya mwezi Januari ili kufikia sheria usawa wa malipo kwa wachezaji. (Sunday Mirror)

Arturo VidaHaki miliki ya picha

Mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Niko Kovac, amekanusha madai kuwa anamezea mate nafasi ya meneja iliachwa wazi Everton, lixcha ya kuonekana Goodison Park siku ya Jumamosi akitazama mchuanao wa klabu hiyo dhidi ya Chelsea ambapo ilipata ushindi wa mabao 3-1. (Goal)
Meneja Jose Mourinho anataka kumsaini beki wa Juventus na Uturuki Merih Demiral kujiunga na Tottenham, na tayari ameungana na Arsenal na Manchester United katika kinyang'anyiro cha usajili wa kiungo huyo wa miaka 21-. (Sun)
Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hajapinga wala kukubali uwezekano wa kuchukua kazi ya umeneja katika klabu ya Arsenal. (TYC Sports via Mail)

Mauricio PochettinoHaki miliki ya picha

Chelsea umeweka dau la £40m kama ofa ya kumnunua mchezaji wa Bournemouth Nathan Ake, 24. (Telegraph)
Liverpool wanamtaka mshambuliaji wa Fluminese Evanilson,20, ambaye atakuwa huru kwa uhamisho bila malipo mwezi Februari. (Netflu via Sun)
Newcastle Unitted wanajiandaa kutengeneza orodha ya wachezaji itakaowasajili mwezi January, huku mshambuliaji wa Hull City Jarrod Bowen, 22, akitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na meneja Steve Bruce. (Telegraph)
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kuwa anamtaka mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 32, asaini kandarasi ya kurefusha muda wake katika klabu hiyo. (Marca)

Lionel MessiHaki miliki ya picha

Mkufunzi wa zamani wa Leicester City Claude Puel amesema "hana tatizo lolote" na Jamie Vardy during his spell in charge, but the 32-year-old England striker sometimes "is like a child" and "needs attention". (Mail on Sunday)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez amefichua kuwa mchezaji mwenzake Wayne Rooney wakati huo alimzawadia gari aina ya Lamborghini baada ya nyota huyo wakimataifa wa Argentina kudhihakiwa na wachezaji wa klabu hiyo kwa kuendesha gari aina ya Audi. (Mail on Sunday)

Post a Comment

0 Comments