BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 04-12-2019

Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumrithi Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Manchester United. (Manchester Evening News)

Tottenham wapo tayari kupokea ofa za usajili za chini ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)
Spurs haina mpango wa kumsajili kiungo Mserbia anayechezea Manchester United Nemanja Matic, 31. (Manchester Evening News)
Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni "uozo" japo "haiwezekani kurudi nyuma". (Mirror)
Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal - in Spanish)
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho
line
Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)
Kocha wa Manchester United Solskjaer amesema anataka klabu hiyo kufanya maamuzi ya haraka katika dirisha la usajili, akiashiria kuwa mwenyekiti mtendaji Ed Woodward hakufanya maamuzi ya haraka mwishoni mwa msimu wa uliopita. (Evening Standard)
Manchester City wameingia katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez. Barcelona pia wanamtaka mchezaji huyo mwenye miaka 22. (Sky Sports Italia, via Calciomercato - in Italian)
Mshambuliaji raia wa Ufaransa Olivier Giroud atafanya mazungumzo magumu na klabu yake ya Chelsea. Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 anataka kuondoka klabuni hapo mwezi Januari. (Evening Standard)
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefanya maamuzi ya kutofanya usajili wowote mwezi Januari licha ya klabu hiyo kupwaya kwenye safu ya ulinzi. (Independent)
Klabu yeyote ya Ligi ya Primia ambayo itataka kumsajili kocha wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez italazimika kulipa fidia ya zaidi ya pauni milioni 20 kwa klabu yake ya sasa, Dalian Yifang ya Uchina. (Mail)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38Haki miliki ya picha
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, anatarajiwa kugoma kurejea katika ligi ya Primia na badala yake kusaini mkataba na klabu yake nyengine ya zamani ya AC Milan. (Telegraph)
Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Arsenal inamtaka nahodha wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta kuchukua mikoba ya kocha aliyetimuliwa Unai Emery. Kwa sasa Arteta ni kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City. (Mirror)
Arsenal ipo tayari, ikibidi, kupitia rekodi na kufanyia usaili mpaka wakufunzi 12 ambao watawania nafasi iliyoachwa wazi na Emery aliyetimuliwa juma lililopita. (Mirror)
Everton wanatarajiwa kutomfukuza kocha wao Marco Silva kabla ya mchezo na mahasimu wao wa jadi Liverpool hapo kesho Jumatano. (Express)
Kocha Manuel Pellegrini amejiongezea muda wa kuifunza klabu ya West Ham baada ya kuifunga Chelsea. Kibarua cha kocha huyo mzoefu pia kipo mashakani kutokana na timu yake kutokuwa na matokeo mazuri. (Mail)
Kocha aliyetimuliwa na klabu ya Tottenham hivi karibuni Mauricio Pochettino amefungua milango ya kurejea katika ligi ya Primia akitamba kuwa yupo tayari kuzamia tena kwenye bahari ya ukufunzi. (Fox Sports, via Mirror)
Mlinzi wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, anaamini Pochettino amekuwa mhanga wa mafanikio yake mwenyewe klabuni hapo na kuwa wachezaji wote wanahisi kusababisha kufutwa kazi kwa kocha huyo raia wa Argentina. (Evening Standard)

Post a Comment

0 Comments