BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO TAREHE 03 -12-2019

Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Arsenal inamtaka nahodha wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta kuchukua mikoba ya kocha aliyetimuliwa Unai Emery. Kwa sasa Arteta ni 


Kocha msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City. (Mirror)
Arsenal ipo tayari, ikibidi, kupitia rekodi na kufanyia usaili mpaka wakufunzi 12 ambao watawania nafasi iliyoachwa wazi na Emery aliyetimuliwa juma lililopita. (Mirror)
Hata hivyo, klabu hiyo inaweza kumpa mkataba wa kudumu kocha wao wa muda kwa sasa Freddie Ljungberg, 42, endapo atafanya mapinduzi makubwa ya matokeo ya michezo yao. (Evening Standard)
  • Kocha wa Everton, Marco Silva
Everton wanatarajiwa kutomfukuza kocha wao Marco Silva kabla ya mchezo na mahasimu wao wa jadi Liverpool hapo kesho Jumatano. (Express)
Kocha Manuel Pellegrini amejiongezea muda wa kuifunza klabu ya West Ham baada ya kuifunga Chelsea. Kibarua cha kocha huyo mzoefu pia kipo mashakani kutokana na timu yake kutokuwa na matokeo mazuri. (Mail)
Katika harakati za kuimarisha kikosi, West Ham wanataraji kusajili golikipa, kiungo na mshambuliaji katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari. (Star)
Kocha aliyetimuliwa na klabu ya Tottenham hivi karibuni Mauricio Pochettino amefungua milango ya kurejea katika ligi ya Primia akitamba kuwa yupo tayari kuzamia tena kwenye bahari ya ukufunzi. (Fox Sports, via Mirror)
Mlinzi wa Tottenham Jan Vertonghen, 32, anaamini Pochettino amekuwa mhanga wa mafanikio yake mwenyewe klabuni hapo na kuwa wachezaji wote wanahisi kusababisha kufutwa kazi kwa kocha huyo raia wa Argentina. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uswidi Zlatan IbrahimovicHaki miliki ya picha

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, anatarajiwa kugoma kurejea katika ligi ya Primia na badala yake kusaini mkataba na klabu yake nyengine ya zamani ya AC Milan. (Telegraph)
AC Milan pia wamepewa ofay a kumsajili mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Calciomercato)
Kiungo mshambuliaji wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, ameweka wazi msimamo wake kuwa hatoingia makubaliano mapya na klabu yake ya sasa na atakataa ushawishi wowote ule utakaolenga kumbakiza Spurs. (Telegraph)
Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson amesema anatumai kuendelea kusalia na mshambuliaji raia wa ays Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, katika klabu hiyo mpaka mwisho wa mkataba wake mwaka 2023. (Sky Sports)
Real Madrid wanajiandaa kutuma ofay a usajili kwa beki wa Napoli na timu ya taifa ya Senegali Kalidou Koulibaly, 28, ambaye amekuwa akiwidwa kwa muda sasa na Manchester United. (Calciomercato)
Klabu ya AS Roma wanajipanga kutunisha ofa ya kumsajili moja kwa moja mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30. Mchezaji huyo kwa sasa yupo kwa mkopo na Roma. (Il Romanista, via Manchester Evening News)

Post a Comment

0 Comments