BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMATATU TAREHE 16-12-2019

Meneja wa muda Freddie Ljungberg amewataka wakuu wa Arsenal kuamua haraka mtu wanaemtaka kuwa meneja wao ajae. (Sun)Hatahivyo, Arsenal bado hawajawasiliana na Wolves kupata ruhusa ya kuzunguza na Nuno Espirito Santo juu ya kazi yao ya umeneja. 
Akikabiliwa na shinikizo meneja Manuel Pellegrini anatarajiwa kuendelea kuiongoza West Ham kwa kemu yao ijayo dhidi ya Crystal Palace itakayochezwa Alhamisi ya baada ya Krismasi. (Guardian)

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji wa Nigeria Josh MajaHaki miliki ya picha

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumhamisha mshambuliaji wa Nigeria anayechezea klabu ya Ufaransa Bordeaux Josh Maja, mwenye umri wa miaka 20, zamani akiichezea Sunderland mwezi Januari. (90min.com)
Chelsea pia wamemuweka mlizi wa Brighton Muingereza Ben White, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amewafurahisha wengi akicheza kwa deni katika Leeds, katika orodha yao wachezaji watakaonunuliwa kwa pauni milioni 25 wakati dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa Januari. (Sun)

Chelsea wanamnyemelea Ben White

Wachezaji wa Bayern Munich wamewaomba wakuu wa klabu hiyo wasaini mkataba na mchezaji nyota wa zamani wa Liverpool Philippe Coutinho, ambaye anacheza kwa mkataba wa mkopo kutoka Barcelona, wakitaka apewe mkataba wa kudumu baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 kuonyesha mchezo mzuri katika mechi dhidi Werder Bremen Jumamosi. (Mirror)
Meneja wa mpito wa Everton Duncan Ferguson atafanya mazungumzo na Moise Kean, mwenye umri wa miaka 19, baada ya kumuondoa uwanjani baada ya kucheza dakika 19 - wakidai mshambuliaji huyo wa Kitaliano alihangaishwa na kasi ya Manchester United. (Telegraph)

Liverpool wamejipanga kufaulu kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na Sam McCallamHaki miliki ya picha

Liverpool wamejipanga kufaulu kinyang'anyiro cha kusaini mkataba na Sam McCallam -kiungo wa nyuma-kushoto wa Coventry kutoka mwezi Januari kabla ya timu nyingine hasimu za Primia Ligi na kumuajiri kwa mkopo Sky Blues kwa kipindi kilichosalia cha msimu. (90min.com)
Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemtaka mshambuliaji wake wa kimataifa Olivier Giroud, mwenye umri wa miaka 33, kuondoka Chelsea mwezi ujao wa Januari lakini mazungumzo na Inter Milan yamekwama. Giroud atakamilisha mkataba wake msimu ujao.(Mirror)

Meneja wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemtaka mshambuliaji wake wa kimataifa Olivier Giroud, aondoke Chelsea.Haki miliki ya picha

Real Madrid wanaendela kumfuatilia kwa karibu winga wa Valencia Muhispania Terran Torres, mwenye umri wa miaka 19. (AS)
Makocha wanaopigiwa upatu kumrithi Unai Emery katika uwanja wa Emirates wanazuiwa na hali ya klabu hiyo kutotaka kununua wachezaji wapya katika dirisha la uhamisho.. (Express)

Aliyekuwa mkufunzi wa Arsenal Unai Emery kabla ya kufutwa kazi na klabu hiyo

Manchester City imeajiandaa kushindana na Manchester United, Liverpool na Chelsea katika kumsajili upya winga wa Uingereza mwenye kwa thamani ya £90m Jadon Sancho, 19. (Sun on Sunday)
Chelsea imeweka dau la 30m euros (£25m) kwa klabu yoyote inayotaka kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Marcos Alonso, 28. (Calciomercato)
Klabu hiyo ya Old Trafford pia inafikiria uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan raia wa Argentina Lautaro Martinez, 22, na kiungo wa kati wa Paris St-Germain Leandro Paredes, 25. (Mirror)

Beki wa kushoto wa Chelsea na Uhispani Marcos Alonso

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Eden Hazard, 28, ameapa kurudi klabu yake ya zamani mkataba wake Real Madrid utakapokamilika . (Sun on Sunday)
Manchester United inafikiria kumnunua mshambuliaji wa Napoli na Ubelgiji Dries Mertens, 32. (Tuttomercato)

Kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 28, anataka kuondoka katika klabu hiyo

Kiungo wa kati wa Chelsea N'Golo Kante, 28, anataka kuondoka katika klabu hiyo lakini atapuuzilia mbali ushauri wa mchezaji mwenza wa Ufaransa Ousmane Dembele, 22, kuelekea Juventus au Real Madrid badala ya Barcelona. (Eldesmarque)
Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho anasema kwamba hatofichua maelezo ya mazungumzo yake na kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen kuhusu hatma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Sunday Mirror

Post a Comment

0 Comments