BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 13-12-2019

Manchester United inaamini kuwa itafanikiwa kumsajili winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, mwezi ujao na huenda pia wakasaini kiungo wa kati wa Tottenham na

Denmark Christian Eriksen, 27. (Mirror) Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na Leeds-mzaliwa wa Norway Erling Braut Haaland, 19, anatafakari kuhusu ofa aliopewa na Borussia Dortmund na RB Leipzig lakini anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United na Juventus kabla ya kuamua hatma yake. (Guardian)
Crystal Palace inataka £80m kumuachilia mshambuliaji wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Chelsea. (Evening Standard)
Wilfried ZahaHaki miliki ya picha
Napoli wanatafakari ofa ya £21m kutoka kwa Arsenal ya kumnunua kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira ikiwa Gunners haitamruhusu kiungo huyo wa miaka 23 kuondoka kwa mkopo mwezi Januari dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa.(Il Mattino - in Italian)
Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, amesema kuwa "anaridhika" kuwa Paris St-Germain, licha ya kutaka kuhama klabu hiyo ya Ufaransa mwanzo wa msimu. (AS)
Kiungo wa kati wa Ubelgiji na klabu ya Shandong Luneng Marouane Fellaini, 32, amepuuzilia mbali tetesi kuwa huenda akahamia Tottenham kujiunga na mkufunzi wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho. (Eleven Sports via Evening Standard)
NeymarHaki miliki ya picha
Tottenham iko tayari kuanza mazungumzo na kipi wa Argentina Paulo Gazzaniga, 27, kuhusu mkataba mpya. (Football Insider)
Kandarasi ya winga wa Chelsea na Uhispania Pedro Rodriguez, 32, inamalizika mwisho wa msimu huu, hatua ambayo huenda ikampatia nafasi ya kuchezea Barcelona kwa mara nyingine. (Sport)
Manchester United haitamuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa mwezi Januari. (Goal.com)
Paul PogbaHaki miliki ya picha
Chelsea huenda ikamnunua tena winga wa Sassuolo na Ivory Coast Jeremie Boga, 22. (Mail)
Barcelona imetuma maafisa wake Milan kujadili mkataba wa Boga. (Sport)
Rangers imemwambia mshambuliaji wa Colombia Alfredo Morelos, 23, kwamba haitamuachilia mwezi Januari. (Football Insider)
Beki wa England Danny Rose, 29, anasema hataki kujadili hatma yake ya baadae na mkufunzi wa Tottenenham Jose Mourinho na kwamba ataendelea mbele na mpago wa kusitisha mkataba katika klabu hiyo. (Mirror)

Post a Comment

0 Comments