BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 06-12-2019

Leicester imeanza mazungumzo na kocha Brendan Rodgers kuhusu mkataba mpya ili kuiwekea ukuta nia ya Arsenal kumnasa kocha huyo. (Telegraph)

Kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino hatakuwa kocha wa Bayern Munich.(Bild)
Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri amesema hatarejea kuwa meneja mpaka kipindi cha majira ya joto lakini anafanya mafunzo ya kiingereza kutokana na kuhusishwa na timu za ligi kuu ya England. (ESPN)
Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili kiungo wa Tottenham Christian Eriksen, 27, mwezi Januari baada ya mchezaji huyo kuwakataa.(Mirror)
Haki miliki ya picha
Mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na timu ya taifa ya Norway Erling Braut Haaland, 19, anaweza kuuzwa kwa kitita cha pauni milioni 17 mwezi Januari kwa mujibu wa mkataba wake.(Manchester Evening News via Bild)
Chelsea wana mpango wa kumsajili mshambualiaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 27, kipindi kijacho cha majira ya joto.(Independent)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud, 33, hataiacha klabu hiyo mwezi Januari huku vilabu vinavyomtaka vikiamua kusubiri mpaka mchezaji huyo atakapopatikana kwa uhamisho wa bure. (Sun)
Borussia Dortmund wana mpango wa kumbakisha mshambuliaji Jadon Sancho, 19 mpaka mwishoni mwa msimu.(Telegraph)
Jadon SanchoHaki miliki ya picha
Kocha wa zamani wa Leicester Nigel Pearson amehojiwa kwa ajili ya nafasi ya ukocha katika klabu ya Watford. (Times)
Kocha wa zamani wa West Ham, Newcastle na West Brom Alan Pardew amesema anapenda kuifundisha Everton lakini amesema kocha wa zamani wa Everton David Moyes 'anafaa kwa nafasi hiyo'.(Mail)
Wakala wa mshambuliaji wa Barcelona KOusamne Dembele,22, amekutana na uongozi wa Chelsea na Manchester City. (El Desmarque - in Spanish)
West Ham watajaribu kumuuza mlinda mlango Roberto mwezi Januari na kutengana na mkurugenzi wa michezo aliyemuingiza kwenye klabu hiyo.(Guardian)
Mshambuliaji wa miaka 17 Ansu Fati ametia saini mkataba mpya wenye kipengele ambacho kitamfanya anunuliwe kwa Pauni milioni 337.5. (FC Barcelona)

Post a Comment

0 Comments