BETI NASI UTAJIRIKE

SIMBA KUMEWAKA MOTO ,MWINGINE TENA AOMBA KUONDOKA

Klabu ya Simba ilitangaza kumfuta kazi mkufunzi wake Patrick Aussems na sasa imeelezwa Kocha wa Viungo, Adel Zrane, ameomba kwenda kwao kwa muda.


Zrane ambaye ni raia wa Tunisia ameaga kwenda kwao kwa ajili ya masuala ya kifahamilia na ikitajwa anaweza kuchukua takribani siku 10.

Maamuzi ya Zrane kuomba ruhusa yamekuja kufuatia timu hiyo hivi sasa haina mchezo wowote ambapo mechi yake ijayo itakuwa dhidi ya Ndanda FC itakayopigwa Disemba 30.

Wakati huo kikosi cha Simba kimekuwa kikiendelea na mazoezi kama kawaida chini ya Denis Kitambi ambaye amekaimu kwa muda nafasi ya Aussems.

Post a Comment

0 Comments