Wiki hii wapenzi wa soka duniani wapo tayari kutazama mechi kati ya Barcelona dhidi ya Real Madrid maarufu sana kama EL CLASSICO ama waingereza waitavyo THE CLASSIC
Mchezo huu wenye historia kubwa duniani umekuwa ukitazamwa zaidi duiani kuliko mchezo wowote . achana na mechi ya Manchester United vs Liverpool, AC Milan vs Inter Milan, Olympic Lyon vs Olympique masseile au hata Simba vs Yanga El Classico inabaki kuwa ni baba la kwa miaka 9 iliyopita Uwepo wa Cristiano Ronaldo na Lionel Messi uliongeza mvuto duniani kwani nyota hao ndio bora zaidi kwa kizazi chetu.
Historia fupi
Mchezo wa kwanza kati ya Barcelona na Real Madrid ulichezwa tarehe 13 Mei 1902 na ulimalizika kwa Barcelona kushinda mabao 3-1.
Timu hizo zimekutana mara 275, Michezo 242 ni mashindano na michezo 33 ni mechi za kirafiki. Barcelona ameshinda michezo 115 kati ya michezo yote.
Rekodi za wachezaji.
Baadhi ya wachezaji wamecheza mechi nyingi zaidi za EL Classico. wachezaji hao ni Sergio Ramos ,Xavi Hernandez, Fransisco Gento na Manuel Sanchis ote wakicheza micheo 42. Sergio Ramos anategemewa kuweka rekodi mpya siku ya jumatano kwa kucheza mechi ya 43 na atakuwa mchezaji aliyecheza mechi za EL Classico nyingi zaidi.
Lionel Messi ndiye mfungaji bora wa El- Classico akifunga mabao 26 kwenye mechi 41. Nafasi ya pili inashikiliwa na Cristiano Ronaldo na Alfredo Di Stefano wote wakifunga mabao 18 kila mmoja.
Wachezaji waliowahi kucheza EL Classico kwa timu zote mbili yaani wamecheza el classico kisha kuhamia Barcelona na kucheza el classico ni 39 wakiwemo Ronaldo De Lima,Luis Figo.
Rekodi za Timu.
Real Madrid imeweka rekodi ya kushinda mabao 11-0 dhidi ya Barcelona . matokeo hayo yalipatikana tarehe 19 Juni 1943 kwenye mchezo wa Copa del Rey na unabaki kuwa mchezo wenye mabao mengi kwa timu hizo tangu kuanzishwa kwake.
kwa upande wa makombe Real Marid imetwaa jumla ya makombe 92 kati ya 96 ya Barcelona.
Itendelea.
0 Comments