BETI NASI UTAJIRIKE

SEHEMU YA 1: VIONGOZI WA SIMBA WAANZA KUTOA SABABU ZA UCHEBE KUTIMULIWA

Klabu ya Simba imemfuta kazi aliyekuwa mkufunzi mkuu wa klabu hiyo Patrick Aussems  pamoja na benchi la ufundi. 


Sisi kama amospoti.com chomb makini cha habari hatukutaka suala hilo litupite bila ufafanuzi makini hivyo tumeanza uchunguzi wa ndani klabuni hapo  kufahau ni lipi hasa limetokea msimbazi . Msemaji wa Simba ndiye aliyenifanya niite makala hii kwa jina tajwa hapo juu . Haji manara kupitia kurasa zake za mitandaoni ameandika hivi

"Waswahili wanaweza kumtupia Senzo mzigo wa lawama. Bodi ya wakurugenzi ndiyo iliyofanya maamuzi, sio Senzo. Hakuna umoja ndani ya timu, timu imegawanyika. Tumefanya maamuzi ili kurekebisha hii hali. Timu ilikuwa inashinda kwa sababu ya uwezo binafsi wa wachezaji"

"Viongozi hawakai na wachezaji kambini. Wajibu wa viongozi ni kuwaonya wachezaji na makocha kama kuna shida. Utovu wa nidhamu umekithiri, viongozi wamejitahidi lakini tabia hiyo inajirudia. Maamuzi haya ni kwa sababu kocha ameshindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji"

"Aussems amewagawa wachezaji makundi makuu mawili. Sasa kocha huwezi kuendesha timu hivyo. Juzi ametoka kumdhihaki mchezaji (Dilunga) bila sababu yoyote."

"Wapo wanaodhani waliofanya uamuzi huu hawipendi Simba. Sio kweli, yaani Mo Dewji haipendi Simba? Bodi ya wakurugenzi hawaipendi Simba?  Haiwezekani Mo Dewji awekeze fedha zake halafu afanye maamuzi yasiyo na tija. Kama timu haina nidhamu haiwezi kusonga mbele"

amospoti.com bado tunaendelea na uchunguzi kufhamu ni nini haswa za kocha huyo kuondoshwa, Haya aliyoyaandika manara ni mageni kwa mashabiki wa soka hasa simba lakini pia yeye amepewa dhamana ya kuizungumzia klabu hiyo hivyo naamini anafuata maelezo ya viongozi. Kaa mkao wa kula tupate kulifahamu suala hili kwa undani.

Post a Comment

0 Comments