BETI NASI UTAJIRIKE

SAMATTA ALAMBA DILI LA MABILIONI ULAYA

Mshambuliaji wa taifa stars na Genk  Mbwana Ally Samatta ameendelea kung'aza zaidi kimataifa si uwanjani pekee Bali hata nje ya uwanja

Samatta amelamba dili nono la ubalozi na amenukuliwa akisema


" Nimesisimka sana kuanza kuwa balozi wa mradi wa 7 Elite Academy.Ni ngumu sana kwa mchezaji yoyote kufikia uchezaji wa kulipwa hivyo nadhamilia kutumia uzoefu wangu kusaidia vijana wenye vipaji wafikie malengo yao.

Kuna mafunzo mengi sana kuhusiana na soka la kulipwa ambayo hayawezi kufundishwa viwanjani hiyo ndio sababu ninafuraha kusaidia 7 Elite Academy kwa upande huo.Hiki ndio kipaumbele changu kama Balozi.

Bila shaka,kujenga msingi endelevu kwa soka la vijana Afrika ya mashariki ni malengo yangu ya awali. Kuna mapenzi makubwa sana ya mchezo kwa eneo na mambo muhimu ambayo yanaweza kubadilisha maisha ndani na nje ya mchezo.

Mipango kwa ajili ya kujiimarisha Tanzania inaendelea na tunaelekea kuiweka wazi hivi karibuni.Sababu ya kuwa na hifadhi za rasilimali za 7 Elite Academy ulimwenguni ni faida kubwa kwa mradi. "Pia siwezi kusubiri kutembelea miradi mingine ya 7 Elite Academy Marekani na Uingereza ,ili niweze kufanya kazi na vijana ambao wana mapenzi ya dhati na soka.Wako tayari kiuhalisia hiyo ndio sababu niliamua kuchukua jukumu hilo. "Inaenda kuwa mradi wa kupendeza kwangu ,kuwa Balozi wa kwanza wa 7 Elite Academy,na nashindwa kusubiri kuanza".

Post a Comment

0 Comments