BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZA SIMBA KUTEMBEZA BAKULI KWA WANACHAMA ZATAJWA

Klabu ya Simba iliwaalika mashabiki wake kutembelea uwanja wake wa mazoezi Bunju B uliojengwa kwa nguvu ya mwekezaji mkuu wa klabu hiyo Mohammed Dewji. 


 Uwanja huo umegawanyika maeneo mawili , eneo la nyasi bandia na nyasi asilia . Wkati wa hafla hiyo ya  matembezi ndipo msemaji wa klabu hiyo alipotangaza mchango maalumu wa kuiwezesha klabu hiyo kujenga ukuta wa tofari kuzunguka eneo hilo. 

Manara amesema ili uzio huo uweze kukamilika ni wajibu wa kila shabiki kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kukamilisha zoezi hilo linalohitaji zaidi ya matofari 90,000. Manara alinukuliwa akisema " 

"Hivi viwanja vimetafutwa kwa nguvu zetu wenyewe wanasimba ,Mwekezaji wetu ametusaiia kuanzisha mradi huu wa viwanja vya uchezea, kawaida wanasimba wanaenda nguvu zao zitumike ndio maana kauli mbiu yetu inasema NGUVU MOJA . 

"Tutaandaa gala kwa ajili ya kumalizia mambo mengine yatakayotakiwa kufanyika ndani ya eneo hilo. Nilizungumza na mwenyekiti na kumwomba suala la kuzungushia ukuta eneo hili ni suala la wanasimba

"Nitaongeza na CEO na mwenyekiti kaduguda tuweke utaratibu maalumu kabla ya gala ili tufanikishe ujenzi wa ukuta maana unaghalimu fedha nyingi sana na unahitaji tofali 90,000 na hii ni haki yetu kuichangia timu yetu  na hili ni lakwetu wanasimba "


Post a Comment

0 Comments