BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZA AUSSEMS KUTIMULIWA ZAWEKWA WAZI HUKU MRITHI WAKE APATIKANA

Klabu ya Simba kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi imethibitisha ujio wa kocha mpya ndani ya klabu hiyo atakaechukua nafasi ya Patrick Aussems iliyokuwa wazi baada  


ya kocha huyo kutimuliwa. Mohammed Dewji ametangaza suala hilo kupitia mkutano mkuu na alinukuliwa akisema 

"Wiki hii, tunaleta kocha mpya, kocha mwenye kiwango kinachostahili kufundisha mabingwa wa nchi hii. Sasa tunaleta kifaa. Mtatangaziwa rasmi, ni nani, na anatoka nchi gani."

Kocha Patrick Aussems aliondoshwa klbuni hapo kwa sababu nyingi lakini kitendo cha kutolewa na UD SONGOkimemuuma mwekezaji huyo na alisema 

"Binafsi bado sijakaa sawa hadi leo baada ya matokeo ya mechi yetu dhidi ya timu ya UD Songo. Nilikuwa sipo nchini. Baada ya mechi ile kuisha, nililia mnoo. "Iliniumiza kupita maelezo. Lakini tumefundishwa katika soka kukubali matokeo yote matatu, ingawa mimi nataka klabu hii, iwekeze katika tokeo moja tu, la ushindi

Post a Comment

0 Comments