BETI NASI UTAJIRIKE

RONALDO AJITETEA JUVENTUS IKIPOTEZA POINTI 2 MUHIMU

Klabu ya Juventus imeshuka mpaka nafasi ya pili kwa mara ya kwanza  kwenye msimamo wa ligi msimu huu wa 2019/20 ikiiruhusu Inter  Milan kuongoza ligi kuu nchini Italy 'Serie A"


Sare ya mabao 2-2 dhidi ya  Sassuolo ilipelekea Inter Milan kuongoza lig kwa tofauti ya pointi 1 baada ya kuifunga Spal mabao 2-1 yaliyofungwa na Lautaro Martinez. Intermilan inajumla ya pointi 37 ikipoteza mchezo mmoja dhidi ya Juventus na sare 1

Kwa upande wa Juventus wao wanapoiti 36 wakiwa hawajaruhusu kufungwa mchezo wowote na sare 3. Mshambuliaji Romelu Lukaku ameendelea kuonyesha makali yake tangu kusajiliwa akifunga mabao 10 kwenye michezo 14 aliyocheza Serie A

Mara baada ya mchezo na Sassulo Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo aliandika " Hayakuwa matokeo tuliyoyataka lakini tutaendelea kuongeza juudi tuweze kufikia malengo yetu"

Kwenye mchezo huo Ronaldo alifunga bao 1 la penati dakika ya 68 huku lile la kwanza kwa upande wa Juventus likifungwa na Bonnuci dakika ya 20. Jeremy Boga alifunga bao dakika ya 22 na Caputo dakika ya 47 kwa upande wa Sassuolo.

Post a Comment

0 Comments