BETI NASI UTAJIRIKE

REKODI MPYA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA KWA MSIMU WA 2019/20

Ligi ya mabingwa imeendelea hapo jana usiku kwa michezo 8 iliyochezwa viwanja tofauti huku 8 zikifanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora zitakazopigwa mwaka 2020 Februari


Moja ya mambo yaliyofurahisha msimu huu ni uwezo wa wachezaji wapya wakiweka rekodi mpya tofauti na hapo awali ilizoeleka kwa wachezaji wawili tu lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Mabao kwa Klabu 

Klabu ya Bayern Munich imeweka rekodi mpya kwenye michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa msimu wa 2019/2020 ikifanikiwa kuhinda michezo yote 6 na kufunga mabao 24 huku ikifungwa mabao 5 tu kwenye mechi hizo. klabu zingine zenye mabao hayo ni Tottenham 18,PSG 17 na Manchester City mabao 16.

Mfungaji Bora 

Lewandowski kutoka Bayern Munich amefunga jumla ya mabao 11 akishindwa kuvuja rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kufunga mabao 12 hatua ya makundi. mbali na mabao hayo Lewandowski anaungana na wachezaji 8 waliofunga mabao 3 kila mmoja . Wachezaji hao ni Haaland, Orsic, Gnabry, Sterling,Mbappe,Rodrygo,Lewamdowski na Milik.

Timu Dhaifu 

Hatua ya maundi ilizikutanisha timu 32 na kati ya hizo timu 7 zimeondoka na pointi chache zaidi. Klabu ya KRC Genk anayoichezea mbwana Samatta ndiyo timu dhaifu zaidi ikipata pointi 1 tu kwenye michezo 6 iliyocheza huku ikifungwa mabao 20 na kufunga mabao 5 tu. Klabu ya Genk inaungana na Galatasary,Club Brugge,Olympiacos,Shakhtar Donestik,Dinamo Zagreb,Bayern Leverkuzen, Lokomotiv Moscow,Redbul,Intermilan ,Slavia Praha ,Benfica ,Zenith,Ajax na Lille.

Rekodi ya Mpya 

Mbwana Samatta ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya mabingwa ulaya. Mchezaji huyo alipata kuwa nahodha wa mechi mbalimbali ligi ya mabingwa ulaya na alifanikiwa kuandika historia ya kuifunga bao klabu ya Liverpool.

Post a Comment

0 Comments