BETI NASI UTAJIRIKE

PATRICK AUSSEMS AMPA UJUMBE MZITO MOHAMMED DEWJI

Aliyekuwa kocha wa Simba Patrick Aussems ameondoka rasmi nchini Tanzania akirejea nchini kwao Ubelgiji. Na kaba hajaondoka Nchini ameandika ujumbe mzito kwa mwekezaji 

na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mohammed Dewji.Aussems ameonekana kusikitishwa na bodi ya utendaji ya klabu hiyo inayoongozwa na Senzo Mazingisa kwa maamuzi ya kumfuta kazi kwa kile kinachoitwa ni utovu wa nidhamu kwa kocha huyo. Patrick ameandika 

"Asante sana wachezaji wote kwa kufanya kazi pamoja ,asante kwa mashabiki kwa sapoti isiyoelezeka. kutoka moyoni nawatakia kila raheli . Nikushukuru Mo kwa kunileta nchi hii nzuri ila kuweza kukua zaidi Simba inatakiwa kujiepusha na wanafiki na wasiokuwa na elimu waliomo ndani ya bodi ambao ndio kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya klabu. Sasa ni wakkati wangu wa kufurahia maisha pamoja na familia yangu. Kwaheri Tanzania"

Post a Comment

0 Comments