BETI NASI UTAJIRIKE

NDANI YA USIKU MMOJA CRISTIANO RONALDO AMJIBU LIONEL MESSI KUTWAA BALLON D'OR

Ukisikia usiku wa vita basi ni huu wa jana.Shirikisho la Soka Ufaransa lilimpa Lionel Messi tuzo ya sita ya Ballon D'OR huku upande wa pili Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo za Serie aKama mchezaji bora wa ligi hiyo kwa mwaka 2019. Ronaldo ametwaa tuzo hizo baada ya kuisaidia klabu yake ya Juventus kutwaa mataji mawili ya Serie A na lile la Copa Italy huku akiibuka mfungaji bora namba 2 kwa Serie A. 

Kwa upande wapili Ronaldo alikuwa ni moja ya wachezaji watatu waliokuwa wanawania tuzo ya Ballon D'or lakini hakutokea jijini Paris kushiriki tuzo hizo na kuamua kubakia nchini Italy zilikoandaliwa tuzo za mchezaji bora wa Serie A na kufanikiwa kushinda tuzo .Kupitia mitandao ya kijamii Ronaldo aliandika

 "Najiskia heshima kuwa mchezaji bora wa Serie A , Nawashukuru wachezaji wenzangu wa Juventus na wachezaji wote walionipigia kura . Mwaka jana ulikuwa ni mwaka wangu wa kwanza Italia na ulikuwa wa kiushindani ila nina furaha na nataka kuufanya mwaka huu uwe sawa na mwaka uliopita"

Post a Comment

0 Comments