Mwenyekiti wa klabu ya Yanga DK. Mshindo Msolla ameshinda nafasi ya ujumbe wa uwakilishi wa klabu za ligi kuu katika bodi ya ligi kwenye uchaguzi uliofanyika jana kwenye
mkutano wa sita wa bodi ya ligi.Msolla alishinda kwa kura 14 za ndio na 4 za hapana huku Herry Nassor akishinda kwa kura 16 za ndiyo na 2 za hapana.
Katika nafasi hiyo iliyokuwa inahitaji wawakilishi watatu walijitokeza wawili ambao ni Dkt. Msolla wa Yanga na Herry Nassory ambaye ni mwenyekiti wa KMC na kura hiz zilipigwa na wajumbe wa ligi kuu tu.
Kwa upande wa wawakilishi wa klabu za daraja la kwanza waliojitokeza watatu huku wakihitajika wawili. Brown Ernest (Mwenyekiti wa Mbeya Kwanza) alishinda kwa kura 34 kati ya 44. Juma Lupangilo(mwenyekiti Ihefu) alishika nafasi ya pili kwa kura 25 huku Abdul Mohammed (mwenyekiti wa African Lyon )akipata kura 14 tu.
0 Comments