BETI NASI UTAJIRIKE

MRITHI WA MWINYI ZAHERA AKOSA NAULI KUTUA YANGA

Baada ya kuondoka kwa Mwinyi Zahera siku chache zilizopita na nafasi yake kukalimiwa na Kocha Boniface Charles Mkwasa mpaka mwisho wa msimu inasemekana baadhi ya makocha wameanza kujipendekeza kwa Yanga akiwemo Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime 

Mexime amesema yeye ni Mwalimu wa mpira na mahala popote anaweza akaenda kama maslahi yanaweza yakiruhusu.

Akizungumza na Radio mojakupitia kipindi cha Michezo, Maxime ameeleza kuwa Yanga bado hawajamtafuta lakini kama watakuja mezani na wakaelewana hataona tabu kuungana nao.

Ameongeza kwa kusema yuko tayari endapo hata atahitajika kufanya kazi nyingine nje ya Ukocha Mkuu ilimradi waweze kuelewana malipo kama atayakubali.

"Mimi ni Kocha, mahala popote nafundisha.Yanga hawajazungumza na mimi, nitakuwa tayari kwenda kama wakishakubaliana nami juu ya maslahi nitakayohitaji.Hata leo naweza kutua Dar, kwa sasa nipo Morogoro, wanaweza tuma nauli pamoja na ya kutolea 'utani' ili nije tumalizane."

Post a Comment

0 Comments