BETI NASI UTAJIRIKE

MOLINGA NA KIKUNDI CHAKE WAZUA TAHARUKI YANGA KISA UKATA

 Uongozi wa Dkt.Msolla na Mwakalebela umeanza kuonja joto la jiwe baada ya taarifa zisizo rasmi kuvuja . Inasemekana wachezaji wa kigeni wameomba kuondoka klabuni hapo 


Ukichana na wachezaji watatu waliokuwa wametajwa hapo awali, inaelezwa pia kuwa Mnamibia Sadney Urikhob naye ameandika barua ya kuachana na Yanga.

Sekeseke la wachezaji wengi wa kigeni Yanga kuondoka limezidi kushika kasi baada ya kuelezwa kuwa David Molinga, Juma Balinya na Lamine Moro kuanzisha suala hilo.

Maamuzi ya wachezaji hao yamekuja kufuatia kudai stahiki zao ambazo ni fedha za mishahara za miezi kadhaa ambazo hazijatolewa mpaka sasa.

Wachezaji hao wa kigeni kwa mujibu wa taarifa wameshindwa kuvumilia kiasi cha kwamba imewapelekea kuandika barua ili waondoke kwa ajili ya kutafuta maisha sehemu zingine.

Tangu kuondolewa kwa kocha mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera klabu hiyo imejikuta ikijiingiza mtegoni kwa kutowalipa wachezaji wake ikiwamo wengine kugoma kucheza akiwemo beki Dante.Bado haijafahamika ni mbinu gani Zahera alizitumia kuwashawishi wachezaji hao kucheza ilihali hawalipwi

Post a Comment

0 Comments