BETI NASI UTAJIRIKE

MOHAMMED DEWJI ATANGAZA BALAA JINGINE BAADA YA UWANJA WA BUNJU KUKAMILIKA

Klabu ya Simba hii leo imefanya mkutano wake wa mwaka 2019 uliowakutanisha mashabiki,wanachama,wachezaji na viongozi wa Simba. Lengo la mkutano huo ni utoaji wa


taarifa kwa klabu ya Simba  na mipango mipya kuelekea mwaka 2020. Mwekezaji mkuu wa klabu hiyo Bw. Mohammed Dewji ametangaza neema kwa timu hiyo

 "Tuna mpango wa kufungua Simba academy ili hapo badae tuje kuvuna vijana waliolelewa kwenye asili ya Simba. Tuwafundishe vijana hao thamani ya Simba na falsafa ya uchezaji wa Simba, na sambamba upendo ili wawe na uchungu zaidi na klabu yetu."
.
"Msimu uliopita ulikuwa mzuri sana kwetu kwa ujumla wake. Kucheza hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika na kisha kuvuka hadi robo fainali ilikuwa ni jambo kubwa kwa klabu, ukizingatia pia tuliweza kutetea ubingwa wetu wa nchi."
.
"Kuzifunga nyumbani klabu kubwa kama Mbabane, Nkana, Soura, Ahly na AS Vita ilikuwa ni heshima kubwa. Hususani tulikuwa tukiwafunga mbele ya mashabiki wetu 60,000 waliokuwa wakituunga mkono kwa hali na mali. Binafsi msimu uliopita ulikuwa amazing."
.
"Niliumia sana kupoteza mechi iliyoandaliwa na wadhamini wetu Sportpesa, ambayo tulicheza na klabu kubwa ya Sevilla kutoka Hispania. Ile mechi tulikuwa tushaongoza kwa idadi nzuri ya magoli, lakini kilichotokea hadi sasa sielewi, lakini ndio football ilivyo
.
"Tulipata shida kidogo katika msimu huu. Nikisema ni bahati mbaya ni utetezi dhaifu, itoshe kusema yaliyotokea msimu huu kwenye #CAFCL ni fundisho kuu kwetu, na nadhani hatupaswi kurudia makosa tuliyoyafanya. Ilikuwa ni aibu kwetu, na tulijiangusha
.
"Binafsi bado sijakaa sawa hadi leo baada ya matokeo ya mechi yetu dhidi ya timu ya UD Songo. Nilikuwa sipo nchini. Baada ya mechi ile kuisha, nililia mnoo."
.
"Iliniumiza kupita maelezo. Lakini tumefundishwa katika soka kukubali matokeo yote matatu, ingawa mimi nataka klabu hii, iwekeze katika tokeo moja tu, la ushindi! "
.
"Mhe mgeni rasmi, mbali ya kutolewa katika #CAFCL, bado sijaridhishwa sana na mwenendo wetu katika ligi ya nyumbani, hata kama tunaongoza ligi. Simba inapaswa icheze kama bingwa mtetezi na kwa soka letu lenye kuburudisha na kutoa matokeo sahihi."

Post a Comment

0 Comments