BETI NASI UTAJIRIKE

MOHAMED DEWJI AWAONYA JONAS MKUDE,CLATOUS CHAMA NA GADIEL MICHAEL CHANZO CHAELEZWA

Mwenyekiti bodi ya wakurugenzi Mohammed Dewji amewatagazia vita wachezaji wakorofi klabuni hapo na ameahidi kuwaondoa endapo wataendelea na tabia hizo. Dewji ametoa 


kauli hiyo kwenye mkutano wa mwaka 2019 uliofanyika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa mwalimu Julius Nyerere. Dewji amenukuliwa akisema 

"Siridhishwi hata tone na nidhamu ya baadhi ya wachezaji wetu nje ya uwanja. Nimekuwa mnyonge kuona uwekezaji tuliouweka kwao, baadhi yao, huutumia kama fimbo ya kutuchapia."
.
"Niwaambie wachezaji wote, Simba ni klabu kubwa kweli kweli, tena kubwa hasa, na hakuna shaka ni namba moja Afrika Mashariki, bodi ninayoiongoza mimi haitavumilia mchezaji yoyote asiyejua thamani ya Simba. Kuonyana onyana sasa imetosha."
.
"Sisi tunawalipa vizuri mno, na wao wana wajibu wa kutulipa matokeo na furaha. Na ili furaha iwepo, lazima nidhamu isimamiwe kikamilifu, na katika hili hatutanii. Hatutajali ukubwa wa jina la mchezaji yoyote."
.
"Nidhamu kwetu ni muhimu kama tunataka tufikie malengo tuliyokusudia. Na haya ndio yaliyotufanya bodi tuchukue maamuzi magumu kwa kocha wetu. Timu imeshindwa kufikia malengo, kisha nidhamu hakuna, alafu tuvumilie?"
.
"Simba lazima tuamue kuteseka na moja katika mambo haya mawili, (1) tuzoee uchungu na maumivu ya nidhamu au (2) maumivu ya matokeo mabaya. Kama mpenzi wa Simba, siwezi"
.
"Simba lazima tuamue kuteseka na moja katika mambo haya mawili, (1) tuzoee uchungu na maumivu ya nidhamu au (2) maumivu ya matokeo mabaya. Kama mpenzi wa Simba, siwezi."
.
"Mtaniwia radhi kidogo nimekuwa mkali ila nidhamu kwangu ndio kila kitu. Hata mimi mwenyewe naishi kwa nidhamu, na ndio siri ya mafanikio yangu, na naamini watu wote waliofanikiwa, na taasisi zote zilizofanikiwa msingi wake mkuu ni nidhamu ya kazi."


"Klabu yetu imeimarisha sana timu zake za vijana na wanawake, na sasa sisi ni miongoni mwa klabu chache Tanzania zenye timu imara za vijana chini ya miaka 20, na ile ya miaka 17, na tuna timu nzuri ya wanawake, na tunazidi kuziimarisha."
.
"Na katika msimu huu wa ligi, tutahakikisha tunachukua tena ubingwa ili tuje kuweka rekodi nyingine kwenye klabu bigwa Afrika. Nawahakikishia wanachama wenzangu kujikwaa si kuanguka, hatutarudia makosa! Insha’Allah, Mungu atutangulie."4


Baadhi ya wachezaji waliotumiwa ujumbe huo ni Mkude,Gadiel Michael na Clatous Chama . wachezaji hawa wamekuwa wakiiingiza kwenye makosa mbalimbali ndani ya klabu hiyo ikiwemo kugoma kusafiri na timu,kutoroka kambini na kutohudhulia/kuchelewa mazoezini.

Post a Comment

0 Comments