Uongozi wa Klabu ya Yanga umewapa wachezaji mapumziko ya siku tatu kabla ya kurejea na kuendelea na maandalizi ya ligi na Kombe la FA.
Wachezaji hao sasa watakuwa wamepewa siku tano za mapumziko baada ya awali kupewa siku mbili.Aidha taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga imethibitisha kuwa wachezaji wa kigeni wamepewa ruhusa maalumukwenda kusalimia familia zao.
Timu itarejea mazooezini siku ya jumatatu 9 2019. Ikumbukwe hapo jana taarifa isiyo rasmi ilivuja na kueleza kuwa Ngasa ,Molinga Balinya na wengine wangeendelea na mazoezi pasipo na mapumziko na ndipo mashabiki walipocharuka mitandaoni na kuomba wachezaji hao wapumzishwe japo kidogo ili wawe fiti zaidi, Uongozi wa Yanga ulipokea maoni na kuwapa likizo hiyo fupi.
0 Comments