BETI NASI UTAJIRIKE

MKWASA AMTAJA ALIYESABABISHA SARE NA KMC

Kocha Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa kuna tatizo kwa waamuzi wa Ligi kuu Tanzania Bara jambo ambalo limemkosesha pointi tatu mbele ya KMC.Hapo jana Yanga ilikubali sare ya kwanza mbele ya KMC ambayo msimu uliopita ilifungwa nje ndani mechi za ligi kuu na kuacha pointi sita kwa Yanga.

Mkwasa amenukuliwa akisema "Tulitengeneza nafasi nyingi na tulishindwa kuzitumia kwani uwezo wetu umeonekana ndani ya uwanja.

"Waamuzi wanamaamuzi yao ila kutakuwa na ulazima wa kuangalia kile ambacho wanakifanya hasa kwenye mechi hizi zenye ushindani mkubwa,"

Yanga jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na KMC uwanja wa taifa, bao lao la kwanza lilifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 73 huku lile la KMC likifungwa na Abdul Hilary kwa mkwaju wa penalti dakika ya 90
+4.

Post a Comment

0 Comments