BETI NASI UTAJIRIKE

MIRAJI ATHUMANI AWATUMIA UJUMBE WANAOTAKA KUTWAA UBINGWA LIGI KUU

Mshambuliaji hatari wa Simba Miraji Athuman amesema kuwa Simba ina nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu.Sheva ambaye ukali wake umeanza kuonekana ndani ya 


Simba kwa msimu wake wa kwanza akitokea Lipuli.pacha  na mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere wamehusika kwenye mabao 17 kwenye jumla ya mabao 19 ya timu hiyo msimu huu. Kagere amefunga nane na kutoa pasi mbili za mabao huku Sheva akifunga sita na kutoa pasi moja ya bao.

Akizungumza na amospoti.com, Sheva alisema kuwa kila mchezaji wa Simba ana ndoto za kutwaa ubingwa wa ligi jambo ambalo  linawafanya wapambane kufikia malengo yao.

Sheva alinukuliwa akisema “Ndoto za wachezaji wote wa Simba ni kuona kwamba tunatetea ubingwa ambao upo mikononi mwa Simba kwa sasa, haiwezi kuwa rahisi ndiyo maana tunapambana kupata matokeo chanya.

“Kikubwa ni kwa mashabiki kuendelea kutupa sapoti bila kuchoka nasi tutafanya kile ambacho wao wanapenda siyo kingine ni matokeo mazuri,”

Simba ipo kileleni ikiwa na pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 10 za ligi, kwa sasa imefungwa jumla ya mabao matatu pekee, timu ya pili ni Kagera ambao wana pointi 24 wakiwa wamecheza michezo 13.

Post a Comment

0 Comments