BETI NASI UTAJIRIKE

MFUPA ULIOMSHINDA MANJI KWA MIAKA 8 ,MO AUTAFUNA KWA MWAKA MMOJA

Klabu ya Yanga itaendelea kujilaumu kwa kipindi kirefu baada ya kushindwa  kumtumia  Yusuf Manji  kwenye maendeleo ya timu hiyo. Manji alijiunga na mabingwa hao wa 



kihistoria kama mwenyekiti wa klabu hiyo na  Manji ameisadia sana Yanga na amejaribu sana kuleta makocha bora, mafunzo na mipango ya safari kwa wanachama wake. 

Wakati Yanga ipo kwenye kilele cha mafanikio Yusuph alijiuzulu badala ya kung’ang’ania madaraka au kutaka kuinunua timu kama ambavyo imekuwa kwa Simba.

Wazee wa Yanga walivyotibua mpango wa Yusuf Manji

Kuna wakati Manji alitangaza kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka kumi na lengo lake ni kuitoa katika mfumo wa wanachama na kuipeleka mfumo wa umiliki kama alivyofanya Mohammed Dewji lakini baraza la wazee wa Yanga likiongozwa na Mzee Akilimali walikataa suala hilo kwa hira zote na wakafanikiwa ikiwamo kumvua Nafasi ya Umakamu mwenyekiti Bw.Clement Sanga na baadae kuvunja jukwaa zima la uongozi

Simba wakubaliana na mfumo mpya 

Wakati Yanga wakimpinga Yusuf Manji upande wa Simba walikuwa wanapambana haswa kuhakikisha timu hiyo inabadili mfumo wa uendeshwaji ikiwemo wanachama kumiliki asilimia 51 na Mohammed Dewji kumiliki asilimia 49. Suala hilo lilikamilika ila kwa shida mno kutokana na uelewa mdogo na upotoshwaji wa baadhi ya wazee kama Mzee Kilomoni.

Mfumo mpya wa Simba wawaumbua Yanga kumtimua Manji 

Moja ya suala la kwanza ambalo Yusuph Manji alikuwa nalo ni ukuzwaji wa Brand ya Yanga kwa Africa na hilo lilikuwa ni rahisi endapo tu wazee wa Yanga wangemkabidhi timu hiyo Yusuph Manji.

Simba wameanza kunufaika na mfumo mpya chini ya Mohammed Dewji kwani timu hiyo kwa mara ya kwanza ilifika hatua ya robor faniali msimu wa 2018/19 na mwaka 2019 imekamilisha ujenzi wa viwanja vya mazoezi pale Bunju.


Mambo aliyoyafanya Mohammed Dewji kwa kipindi cha miaka miwili yamemfanya Manji aonekane si chochote kwenye soka la Tanzania kwa kipindi chote alichokaa klabuni hapo. Binafsi simu]laumu Manji bali viongozi,wazee na hata mashabiki wa timu hiyo hawakuwa na jambo lolote jema kwa tajiri huyo


Post a Comment

0 Comments