BETI NASI UTAJIRIKE

MFAHAMU MCHEZAJI MSOMI ZAIDI WA KLABU YA SIMBA

Dirisha kubwa la usajili kwa msimu wa 2019/20. Simba ilifanikiwa kusajili wachzaji wa kimataifa kwa ajili ya kuja kuiongezea nguvu safu ya kiungo ya timu hiyo. moja ya wachezaji
 hao ni Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman ambaye alijiunga na timu hiyo akitoka Al Hilal inayoshiriki Ligi Kuu ya Sudan.

Ujio wa Shiboub katika kikosi cha Simba ulipokelewa kwa mikono miwili na mashabiki wa timu hiyo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza soka.

Mchezo wake wa kwanza kuitumikia timu hiyo mbele ya mashabiki ilikuwa ni dhidi ya Power Dynamos ya Zambia uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mechi hiyo ilikuwa ni ya mchezo wa kirafiki wa Simba Day na alionyesha uwezo wa juu.

Lakini pia, kama haitoshi Shiboub aliwapagawisha vilivyo mashabiki hao wa Simba katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Katika mchezo huo, Shiboub alifanikiwa kuifungia timu yake hiyo mabao mawili kati ya manne iliyoshinda. Hali hiyo iliwavutia zaidi wapenzi na mashabiki Simba na kuzidi kuwa na imani naye.

Hata hivyo, licha ya ufundi huo wa kutandaza soka uwanjani, kuna jambo jingine kubwa ambalo mashabiki walio wengi wa Simba wanaweza wasilijue kuhusiana na nyota huyo.

Kama ni mmoja kati ya watu hao basi amospoti.com linakujuza kuhusiana na Shiboub mwenye urefu wa mita 1.82. Ukizungumzia wachezaji wasomi wanaoshiriki Ligi Kuu Bara msimu huu, basi jina la Shiboub huwezi kuacha kulitaja.

Shiboub ambaye amezaliwa, June 7, 1994 huko nchini Sudan na ambaye sasa ana miaka 25, ni msomi mwenye degree (Shahada) ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Information Technology). Degree hiyo ameipata katika Chuo Kikuu cha Sudan kabla ya kujikita rasmi katika mchezo wa soka.

Shiboub anasema kuwa aliamua kusoma masomo hayo ili atakapoachana na soka aweze kuwa na kazi nyingine ya kufanya kwa ajili ya maisha yake ya baadaye.

Shiboub alinukuliwa akisema “Soka ni mchezo wa muda mfupi tu, kwa hiyo niliamua kusoma masoma haya ya IT ili nitapoachana na soka, niweze kuwa na kazi ya kufanya.

“Niliamua kusomea fani hii ya IT kwa sababu ni moja kati ya fani nilizokuwa nazipenda sana kutoka moyoni.

“Hata hivyo, kuna changamoto nyingi ambazo nilikumbana nazo wakati nikisoma lakini sikuweza kukata tamaa na hatimaye niliweza kuhitimu.

“Naamini nitakapoachana na soka fani yangu hii itanisaidia katika kukabiliana na changamoto nyingine za maisha,” 

Post a Comment

0 Comments