BETI NASI UTAJIRIKE

RASMI : SULEIMAN MATOLA ATEULIWA KUINOA SIMBA MSIMU WA 2019/20

Klabu ya Simba imetangaza rasmi kumpa nafasi ya ukocha msaidizi aliyekuwa kocha wa Polisi Tanzania Suliman Matola anayekaimu nafasi ya Kitambi aliyepelekwa


 timu ya vijana . Simba wamefikia kuvunja benchi la Ufundi kwa kumuondoa Patrick Aussems na jopo lake huku Suleiman Matola akiwa ni kocha wa kwanza kusajiliwa klabuni hapo.Watu wengine wanaotajwa kuwaniwa kuliunda benchi la Ufundi ni Musa Hassan Mgosi .

Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara amethibitisha uteuzi wa Matola huku akisema ujio wa kocha Mkuu upo njiani na watamtangaza siku chache zijazo.

Msemaji huyo amezikataa shutuma za baadhi ya watu wakidai timu hiyo imeshindwa kumlipa Patrick Aussems ndiyo maana aliondolewa klabuni hapo na manara ameendelea kusistiza sababu za kuondolewa Aussems ni Makosa ya kinidhamu aliyoyaonyesha pamoja na kushindwa kufuzu hatua ya Makundi ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments