BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED YAICHINJILIA MBALI TOTTENHAM YA MOURINHO

Ligi kuu nchini Uingereza imeendelea hapo jana usiku kwa michezo mbalimbali huku mchezo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu ni kati ya Manchester United dhidi ya TottenhamManchester United ilioyesha uwezo wa hali ya juu kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Manchester United iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 huku mfungaji mahili Rashford akiibuka nyota wa mchezo huo kwa kufunga mabao yote mawili na lile la totenham likipatikana kupitia Dele Alli

Manchester United ilionekana kuukamia mchezo huo kwa dakika zote 90 ili kulinda kibaru cha kocha wao Ole Gunnar anayeweza kutimuliwa wakati owote kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Mechi Kamili

Mchezo huo ulipigwa dimba la Old trafford majira ya saa 4:30 huku manchester United ikiwaanzisha nyota wake David Degea, Maguire,Ashley Young,Wan Bissaka,Mc Tominay,Fred,Lingard ,James ,Green Wood na Rashford  huku Tottenham akianza mchezo huo kwa kuwatumia  Gazzaniga,Auriel,Vertonghen,Sissoko,Winks,Alli,Son,Lucas na Kane

Marcos Rashford aliipa Manchester United bao la kuongoza dakika ya 6 lakini bao hilo halikudumu kwani Dele Alli alisawazisha dakika ya 39 mpira ulikwenda mapumziko kwa timu hizo kwenda Sare ya mabao 1-1.

Dakika ya 48 ya Mchezo Marcos Rashford aliangushwa ndai ya 18 na kupata penati aliyoipiga kwa umakiNi na kupata bao la pili.

Kwa matokeo hayo Manchester United imepanda nafasi tatu za juu kutoka namba 9 hadi 6 ikiwa na pointi 21 kwa kucheza michezo 15.Post a Comment

0 Comments