Klabu ya Manchester United imeweka rekodi mpya kwenye mchezo wa UEFA EUROPA LEAGUE kwa kufanikiwa kushinda mabao 4-0 dhidi ya AZ Alkmaar kwenye mchezo wa
mwisho wa kundi L . Manchester United imefuzu hatua ya 32 bora na kungojea kupangwa hatua ya mtoano. Klabu hiyo imetinga hatua ya mtoano ikiwa ni klabu iliyofungwa magoli machache zaidi kwenye michezo 6 iliyocheza. Manchester United imeruhusu mabao 2 tu na kufunga mabao 10.
Klabu hiyo ilishinda mabao 4-0 dhidi ya AZ Alkmaar na mabao hayo manne yalifungwa na wachezaji 3 tofauti ndani ya dakika 11 za mchezo . Ashley Young mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye kikosi hicho alifunga bao la kuongoza dakika ya 53 ya mchezo, Greenwod akifunga mabao dakika 58 na 64 huku Juan Mata akifunga bao dakia ya 62 kwa mkwaju wa penati.
Kikosi cha manchester United kilikuwa na Sergio Romero, Ashley Young ,Tuanzebe ,Maguire ,Williams,Garner ,Nemanja Matic,Green wood, Juan Mata, Pereira na Antonio Martial
0 Comments