BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA ALUSHA DONGO JINGINE KWA YANGA WAKATI WA UZINDUZI WA BUNJU COMPLEX

Mashabiki wa klabu ya Simba kwa mara ya kwanza walifanya matembezi maalumu ya kuona viwanja vyake vya mazoezi vilivyopo bunju. Kwenye matembezi hayo kulikuwa na mwamko mkubwa wa mashabiki wa klabu hiyo. Wegi walionekana kufurahishwa na utendaji mzuri wa bodi ya Simba ikiongozwa na mwekezaji wake Mohammed Dewji. Matembezi hayo yalizaa matunda hususani kwenye awamu ya pili ya ujenzi inayotegemewa kuanza hivi karibuni.

Msemaji wa klabu hiyo alinukuliwa akisema "Mwekezaji wetu Mohammed Dewji amefanikiwa kujenga viwanja hivi lakini pia sisi kama wanachama tunapaswa kuchangia kidogo ili tukamilishe ujenzi wa ukuta wenye uhitaji wa matofari 90,000 hiyo kila mwanasimba anawaji wa kuchangia hilo, Nitaongea na CEO kujua tunaweka utaratibu mzuri wa kufanikisha hilo na hatutakiwi kuwa kama wale wenzetu (Yanga) maana walizoea kubebwa lakini saa hizi mbeleko imekatika na wao chali"

Post a Comment

0 Comments