BETI NASI UTAJIRIKE

LIONEL MESSI AWEKA REKODI MPYA BALLON D'OR

Hatimaye mshambuliaji wa Barcelona na Argentina amefanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji bora wa Dunia Ballon D'OR kwa Mwaka 2019 akiwamwaga Cristiano Ronaldo na Van Dijk


Lionel Messi anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza duniani kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya Sita akimwacha mpinzani wake Cristiano Ronaldo mwenye tuzo 5.

Messi alitwaa tuzo ya kwanza ya FIFA Ballon D'or mwaka 2009 kisha 2010,2011,2012 ,2015 na sasa ametwaa tuzo ya Ballon D'or  mwaka 2019. Messi mwenye miaka 32 amekuwa mwiba mkali kwa mwaka 2019 akifunga mabao 36 na kuisaidia Barcelona kutwaa La Liga.

Klabu ya Barcelona  imeifikia rekodi ya Real Madrid kwa kutwaa Ballon D'OR nyingi huku timu hizo zikitwaa tuzo hizo mara 11 kila moja . Real Madrid imetoa wachezaji 7 huku Barcelona ikitoa wachezaji 6 waliowahi kutwaa tuzo hiyo.

Klabu za Juventus na AC Millan zimetwaa tuzo hizo mara 8 kila moja huku Bayern Munich ikitwaa tuzo hizo mara 5 na Manchester United ikitwaa tuzo hizo mara 4 ikiwemo moja ya mchezaji Cristiano Ronaldo mwaka 2008.

Kwa Upande wa wachezaji tuzo hiyo inashikiliwa na Lionel Messi akitwaa mara 6 , Cristiano Ronaldo mara 5 ,Michel Platini mara 3 ,Johan Cruffy 3 na Marco Van Basten 3.

Post a Comment

0 Comments