BETI NASI UTAJIRIKE

KUNA KIONGOZI YEYOTE ALIYEWAHI KUWA BORA KAMA MOHAMMED DEWJI PALE SIMBA?

Klabu ya Simba kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake inakwenda kuzindua uwanja mpya wa mazoezi uliojengwa na mwekezaji wa klabu hiyo bwana Mohammed Dewji 



Mohammed Dewji alitoa ahadi ya ujenzi wa viwanja vya ichezo kwa ajili ya klabu hiyo na sasa ametekeleza kwa vitendo. Wakat waa uzinduzi wa ujenzi wa viwanja hivyo uliyofanywa  na waziri Mwakyembe kila mtu alidhani suala hilo lingechukua miezi mingi.

Mohammed Dewji amedhihirisha nini maana ya kuwekeza ,kitendo cha kujenga uwanja wa mazoezi,kitendo cha kuwapa kambi ya hadhi  wachezaji wa simba,kulipa  wachezaji hao kwa wakati na mishahara inono ni dhahiri mwekezaji huyo amedhamilia kuipeleka Simba kimataifa zaidi.

Simba ilianzishwa mwaka 1935 ila kitendo cha kutokuwa na viwanja ,Akademi,Hostel na hata vitega uchumi vya kueleweka ni dhahili klabu hiyo iliongozwa na wajanja waliofikiria zaidi matumb yao na si maendeleo ya klabu hiyo.

Post a Comment

0 Comments