BETI NASI UTAJIRIKE

KIONGOZI AWAPA MAJUKUMU MAZITO WACHEZAJI SIMBA KUELEKEA MECHI NA YANGA

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Abdallah King Kibaden, amesema anatamani kuona rekodi yake inavunjwa na wachezaji wa timu hiyo waliopo hivi sasa.


Kibaden ameeleza kwa mabadiliko yanayoendelea hivi sasa ndani ya klabu ya Simba yatawawezesha wachezaji kupata nguvu ya kuzidi kupambana na kuonesha cheche ndani ya timu.

Rekodi inayokumbukwa na ambayo haijavunjwa mpaka sasa ni mabao matatu aliyoyafunga katika mechi ya watani wa jadi mwaka 1977 Simba ilipoibuka na ushindi wa mabao 6-0 ambao haujalipwa mpaka sasa.

"Kwakweli natamani kuona vijana wakivunja rekodi yangu.Kwa mwenendo huu ambao Simba inaelekea kukamilisha mfumo wa mabadiliko naamini watakuwa na kila nyenzo ya kufanya vema.Nataka kuona mchezaji akivunja hii rekodi na itakuwa rekodi nzuri kwangu.

Ujumbe huu unawalenga wachezaji Meddie Kagere na Miraji athumani ambao ni wachezaji tegemezi wa klabu hiyo wakiwa wamc=efunga jumla ya mabao 16 kwenye michezo 10 waliyocheza

Mchezo wa raundi ya kwanza kati ya Simba na Yanga unategemewa kuchezwa tarehe 4 Januari 2020 katika dimba la Taifa "Kwa Mkapa"

Post a Comment

0 Comments