BETI NASI UTAJIRIKE

KIBOKO YA MOLINGA NA KAGERE AMEANZA KUONYESHA CHECHE ZAKE BIASHARA UNITED

Mshambuliaji hatari raia wa Nigeria aliyesajiliwa na Biashara United wiki chache zilizopita ameanza kuonyesha hatari yake baada ya kucheza mchezo mmoja wa ligi kuu dhidi ya 
Ndanda FC na kufanikiwa kufunga bao pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 walioupata. Mshambuliaji huyo anafahamika kwa jina la Obinna aka Zlatan aliwasili nchini Tanzania mwezi Novemba akitokea mapumziko nchini kwao Nigeria. 

Mshambuliaji huyo anategemewa kung'ara zaidi ligi kuu msimu huu hasa  kuanzia Januari 2020 baada ya  Ligi kuu Tanzania kusimama kupisha michuano ya CECAFA UGANDA kwa mwaka 2019.

Obina (Kushoto ) akiwa na meneja wake Kabir Danjuma 

Meneja wa mchezaji huyo Danjuma Kabir alinukuliwa akisema:

" Obina ni straika mwenye nguvu,mbunifu na anauwezo mzuri wa kumiliki mpira na kufunga ,uwepo wake ndani ya Biashara United naamini ni baraka kwao na kama watamtumia vyema basi atawasaidia kujikwamua kwenye nafasi za chini kabisa kwenye msimamo wa ligi

"Nimewaona baadhi ya mastraika wanaoshiriki ligi kuu Tanzania Bara na Obina ni aina ya mastraika kaliba ya Meddie Kagere na David Molinga. kwa upande mwingine  amewazidi washambuliaji hao baadhi ya vitu ikiwemo kuanzisha mashambulizi na kucheza nafasi mbali mbali uwanjani" 

Kwa upande wa mchezaji Obinna ameahidi makubwa kwa viongozi na mashabiki wa timu hiyo na alinukuliwa akisema 

"Malengo yangu ni kufanya vizuri zaidi msimu huu. Nawashukuru wachezaji na makocha kwa mchezo mzuri tuliouonyesha  dhidi ya Ndanda ha tulistahili kushinda"

Kwa Sasa Biashara United imecheza michezo 13 ikipata pointi 15 na uwepo wa mchezaji Obinna utawasaidia kutoka nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi kuu na kupanda zaidi.


Post a Comment

0 Comments