BETI NASI UTAJIRIKE

JURGEN KLOPP ALALAMIKIA HUJMA TUZO ZA BALLON D'OR

Kocha wa Liverpool Jurgen klopp ameonekana kutofurahishwa na utolewaji wa tuzo za Ballon D'or zilizotolewa hapo juzi jijini Paris Ufaransa na Lionel Messi kutwaa tuzo hizo


Kwenye orodha ya wachezaji 10 klabu ya Liverpool iliingiza wachezaji 4 akiwemo Mo Salah,Allison Bekker aliyetwaa tuzo ya kipa bora,Sadio Mane na Virgil Van Dijk aliyeshika nafasi ya pili kwenye tuzo hizo.

Awali Klop alinukuliwa akisema " Lionel Messi ni mchezaji bora duniani ila kwa msimu huu hastahili tuzo" kocha huyo alikuwa akimpigia chapuo beki wake Van Dijk aliyetwaa tuzo mbali mbali ulaya ikiwemo tuzo ya beki bora Uingereza, Mchezai bora wa msimu Uingereza na alifanikiwa kuipa Liverpool kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na kuisaidia Uholanzi kufika fainali michuano ya UEFA NATIONAL LEAGUE  mchezo waliopoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Ureno.

Mara baada ya Lionel Messi kutangazwa mchezaji bora kwa mara ya sita Jurgen Klopp alinukuliwa akisema 
"Maamuzi si yamefanywa na wanahabari? inaona tofauti, Messi ni mchezaji mzuri ila kwa msimu uliopita hakuna mchezaji alikuwa bora kama beki wetu. Naweza kuwa sahihi kusema Virgil alistahili kushinda tuzo ile kwani tuishinda Championi Ligi na alikuwa na msimu mzuri"

Messi alimzidi Van Virgil kwa kura 6 tu akipata kura 686 na Van Virgil kupata pointi 679. Van Virgil ameendelea kuwa beki bora msimuu huu kwa kuiwezesha liverpool kungoza ligi kuu Uingereza kwa pointi 40 kwenye michezo 14 huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote w ligi.

Post a Comment

0 Comments