BETI NASI UTAJIRIKE

IFAHAMU REKODI YA MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA ALIYETOKEA MISRI

Zikiwa zimesalia siku tatu ili dirisha dogo la usajili liweze kufunguliwa Klabu ya Yanga imeshaanza kukusanya wachezaji watakaotumika raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara Hapo jana katibu mkuu wa Yanga  DK.David  Ruhago alimpokea mshambuliaji Tariq Seif Kiakala akitokea Misri .Dirisha dogo la usajili litafunguliwa tarehe  16 Disemba mpaka 15 Januari 

Tariq anatarajiwa kusaini mikataba na mabingwa hao wa kihistoria mara baada ya dirisha dogo kufunguliwa. Mshambuliaji huyo amewahi zitumikia klabu za Biashara United na Stand United kabla ya kutimkia klabu ya Dekernes FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri. 

Mshambuliaji huyo anatajwa kuchukua nafasi ya Balinya ambaye amevunja mkataba na kuondoka klabuni hapo . 


Rekodi ya Tariq msimu wa 2018/19 akiwa Biashara United 

Mchezaji Tariq   aliwahi kufikisha  magoli matano ndani ya mechi nne alizocheza  kwenye ligi kuu Bara 
Alifunga dhidi ya Lipuli FC Biashara ikishinda 3-0.
Akafunga dhidi ya Yanga Biashara ikishinda 1-0.
Akafunga dhidi ya Alliance Biashara ikifungwa 2-1.
Akafunga mabao mawili dhidi ya  Ruvu shooting Biashara ikishinda  2-0 Ruvu Shooting.

Post a Comment

0 Comments