Mshambuliaji wa Barcelona Lioel Messi ameendelea kuweka rekodi mpya baada ya hapo jana kufunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya RCD Mallorca .
Magoli hayo matatu yanamfanya Lionel Messi kuwa na Hat trick 35 kwenye La Liga akimwacha aliyekuwa mpinzani wake wa La Liga Cristiano Ronaldo mwenye hat trick 34 kwenye La Liga .
Kwa msimu huu mpinzani wa Lionel Messi atakuwa Karim Benzema kwani mpaka sasa ana mabao 11 huku Lionel Messi anayeongoza akiwa na mabao 12. Benzema amekuwa na msimu mzuri zaidi kwa mwaka huu tangu kuondoka kwa Cristiano Ronaldo.
Kwa upande wa timu za Real Madrid na Barcelona zimeendelea kuchuana vikali kuelekea kutwaa kombe la la liga huku zote zikicheza michezo 15 na kupata pointi 34 huku zikitofautiana kwa mabao 2.
Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Mallorca na kuufanya muunganiko wa Lionel Messi,Griezman na Suarez kuanza kuwa tishio. Kwenye mchezo huo Antonio Griezman aliipatia Barcelona bao la kuongoza dakika ya 7 ,Lionel Messi 17,41,83 huku Suarez akufunga bao dakika ya 43 kwa upande wa Mallorca Ante Mudimir alifanikiwa kufuga mabao mawili dakika ya 35 na 64
0 Comments