BETI NASI UTAJIRIKE

HUU NDIO MWISHO WA OLE GUNNAR SOISKJAER PALE MANCHESTER UNITED?

Klabu ya Manchester United imeendelea kuwa na mokeo mabaya zaidi kwa msimu huu wa 2019/20 ikicheza mechi 14 na kupata pointi 18 na kushika nafasi ya 9 ikishinda michezo 5 


sare 5 kufungwa 4 n huu ni mwanzo mbaya zaidi kwa kocha huyo. Wiki ijayo anacheza michezo miwili migumu kati ya Tottenham na Manchester City. Ukiziangalia timu hizo kwa sasa zimekuwa zikifanya vyema. Guardiola anataka kutetea  ubingwa baada ya kuanza vibaya msimu akiruhusu Liverpool kumuacha kwa pointi 11.

Tottenham ilianza msimu huu kwa kusua sua na kupoteza michezo mingi ndipo tukashuhudia bodi ya klabu hiyo kumfukuza kocha wake Mauricio Pochettino na mikoba yake kukabidhiwa Jose Mourinho aliyeiongoza kwenye michezo mitatu na kushinda yote ukiwemo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Bado haijawekwa wazi endapo timu hiyo itapoteza michezo hiyo miwili migumu. Wiki iliyopita ilikuwa ni ngumu kwa klabu hiyo baada ya kutoka sare na Shiffield United kwa mabao 3-3 kisha kufungwa mchezo wa Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Astana 2-1 na hapo jana ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Aston Villa.


Post a Comment

0 Comments