BETI NASI UTAJIRIKE

HII NDIYO SABABU ILIYOPELEKEA KIFO CHA ALLY YUSUFU "TIGANA "

Mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’ amefariki  jana katika hospitali ya Amana mjini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu, Mwanamtwa Kihweli msiba upo nyumbani kwake Kimara na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kikao cha wanandugu.


Mkewe alikuwa anaumwa ikabidi akarudi kwao Ilala, naye akaja kumuona mkewe juzi ndio ghafla akaanza kuumwa tumbo la kuhara akapelekwa Amana hadi umauti umemkuta leo,


amesema Kihwelo ambaye amecheza pamoja na Tigana, Yanga, Simba kote mara mbili na Cadets ya Mauritius. 

Tigana alizaliwa mwaka 1970 Ilala mjini Dar es Salaam na amekulia Mtaa wa Saadani huku akisoma shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko ambako ndiko alianzia soka kama kipa na baadaye mchezaji wa ndani.

Timu yake ya kwanza ni Shaurimoyo Kids kabla ya kujiunga na Manyema Rangers mwaka 1989 ambako alicheza hadi mwaka 1991 alipochukuliwa na Pan Africans ikiwa Daraja la Pili (sasa Daraja la Kwanza) wakaipandisha Ligi Kuu mwaka 1993.

Mwaka 1994 akachukuliwa na Yanga SC ambako alicheza kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Simba SC alikocheza hadi mwaka 1997 akaenda Cadets ya Maurtius alikocheza hadi mwaka 2000 aliporejea Simba SC. 
  
Alicheza kwa msimu mmoja Simba SC kabla ya kurejea Yanga SC ambako alicheza hadi mwaka 2004 alipokwenda kumalizia soka yake Twiga SC ya Kinondoni. Jina la Tigana alipewa kutokana na kufananishwa na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa miaka ya 1980, Jean Pierre Tigana.

Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’.

Post a Comment

0 Comments