BETI NASI UTAJIRIKE

HABARI MPYA KUHUSU POGBA KUELEKEA MCHEZO NA TOTTENHAM

Kocha wa Manchester United amethibitisha kukosekana kwa kiungo wake muhimu Paul Pogba kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Tottenham Hotspurs Pogba amekuwa nje ya uwanja tangu mwezi Oktoba alipocheza mchezo wake wa mwish dhidi ya Arsenal kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya mabao 1-1.  Klabu ya Manchester United imekuwa kifanya vibaya zaidi msimu huu na kukosekana kwa Pogba limekuwa pigo kubwa kwa timu hiyo.

Pogba anamajeruhi kwenye eneo la enka na haijawekwa wazi ni lini atakuwa atarejea uwanjani. Kocha mkuu wa Manchester United amenukuliwa akisema 

"Pogba hatutakuwa nae ila ameanza mazezi mepesi kuweza kurejea dimbani" Mchezo kati ya Manchester United na Tottenham Hotspurs utapigwa leo usiku wasaa 4:30 kwenye dimba la Old Trafford huku macho yakiwa kwa kocha Jose Mourinho aliyetimuliwa na Manchester United mwaka 2018 na sasa ataiongoza Tottenham kuwakabili Manchester United 

Post a Comment

0 Comments