BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS 12-12-2019

Everton imezungumza na ajenti wa Mino Raiola kumuachilia mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, ikiwa yuko tayari kuhamia Goodison Park, japo AC Milan inapigiwa 
upatu kumsani mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United. (Arena Napoli, via Sport Witness)
Naibu mkufunzi wa Manchester Mikel Arteta angependelea sana kurejea katika klabu yake ya zamani ya Arsenal kama maneja wake mpya lakini anataka hakikisho kutoka kwa wasimamizi wa klabu hiyo. (Sun)
Arsenal na Everton ziko tayari kukutana na mkufunzi wa zamani wa Chelsea Carlo Ancelotti, baada ya kufutwa kazi usiku wa Jumanne. (Evening Standard)

Carlo AncelottiHaki miliki ya picha

Bilionea wa Marekani Todd Boehly, ambaye ni miongoni mwa wamiliki wa Angeles Dodgers, anatafakari uwezekano wa kununua Chelsea, licha ya wasimamizi wa klabu hiyo kusisitiza hakuna mpango wa kuiuza. (Telegraph)
Manchester United imeonesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji wa Bayer Leverkusen Mjerumani Kai Havertz, 20. Hatahivyo inakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Barcelona, Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich. (Bild, via Express)
Mkufunzi wa muda Duncan Ferguson, 47, hataki kazi ya kuwa meneja wa kudumu wa Everton, licha ya kuinyuka Chelsea mabao 3-1 katika mechi yake ya kwanza. (Liverpool Echo)
Kocha wa Chelsea Frank Lampard anajiandaa kumnunua winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27,mwezi Januari. (Mirror)

Olivier GiroudHaki miliki ya picha

Inter Milan na Atletico Madrid ni miongoni mwa vilabu vinavyomnyatia Olivier Giroud huku mshambuliaji huyo wa Ufaransa wa miaka 33-akiwa tayari kondoka Chelsea mwezi January. (Football.London)
West Ham huenda ikampiga kalamu mkufunzi wake Manuel Pellegrini, 66, ikiwa Hammers itashindwa na Southampton Jumamosi hii. (Sun)
Chelsea imewatuma wasaka vipaji wake kufuatilia mchezo wa mshambuliaji mfaransa Moussa Dembele, 23, na mshambuliaji wa RB Leipzig Timo Werner, 23, usiku wa Jumanne (Mail)
Juventus wameripotiwa kuwa na mpango wa kumnunua beki wa kushoto na kulia wa Chelsea na Italy Emerson Palmieri, 25, msimu ujao. (Tuttosport, via Football Italia)

Juventus wameripotiwa kuwa na mpango wa kumnunua beki wa kushoto na kulia wa Chelsea na Italy Emerson PalmieriHaki miliki ya picha

Rangers inakabiliwa na hofu ya kumpoteza winga wake wa miaka 17 Mskochi Kai Kennedy huku Bayern Munich na Manchester City zikiwa miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsaini. (Daily Record)
Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na West Brom Carlos Vela, 30, ananyatiwa na Barcelona. Mshambuliaji huyo wa Mexico kwa sasa anachezaa katika klabu ya Los Angeles FC inayoshiriki Major League Soccer. (Goal)
Kocha mkuu wa usakaji wa vipaji katika klabu ya Manchester United Marcel Bout alikuwa akitazama mechi ya klabu bingwa Ulaya kati ya Red Bull Salzburg dhidi ya liverpool siku ya Jummanne huku mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 19, akiwa ndio lengo lake . (Sky Sports)
Mshambuliaji wa Everton Moise Kean, 19, huenda akarejea Italia miezi sita tu baada ya kujiunga na klabu hiyo huku Bologna ikimtaka kwa mkopo. (Star)

Post a Comment

0 Comments