CV YA KOCHA MPYA WA SIMBA YAGEUKA GUMZO KWA MASHABIKI WA SOKA TANZANIA

Klabu ya Simba limtangaza Sven Vandernbroeck kuwa kocha mkuu wa Simba akichukua nafasi ya Mbeligiji mwenzake Patrick Aussems. Kocha huyo ameibua hisia tofauti miongoni 



mwa wadau wa soka nchini huku wengi wakihoji ubora. wa Kocha huyo. Amospoti.com iliamua kuingia chimbo kutafuta CV ya kocha huyo.

1. MAFANIKIO

2017 – Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON)- Gabon akiwa na timu ya
Taifa ya Cameroon. Kushirikia michuano ya Shirikisho Urusi.

2014/15- Aliipeleka Daraja la Kwanza 0H Leuven (Pro- League).

2013/14- Aliifundisha Fostiras na kuweka rekodi ya kutofungwa katika mechi 13 akishinda 10 na kutoa sare tatu. Aliruhusu bao moja pekee katika raundi ya pili akiwa na timu hiyo wachezaji wake wakiwa na umri wa miaka 21, walicheza mechi playoff ilikupanda, lakini bajeti ya ligi ilikuwa ndogo.


2. ELIMU
2014- Alipata leseni ya juu kabisa ya Uefa (Pro Licence), Brussels- Ubelgiji.
2012- Alipata leseni A ya Uefa, Brussels- Ubelgiji.
2003- Alipata leseni B ya Uefa, Uholanzi.


3. KOZI ZA ZIADA
2011- RSC Anderlecht- Modern Football siku moja.
2012- Manchester City- Mancini (Italia) siku nne.
2014 -Olympiacos- Michael (Hispania) siku nne.
2016-University Leuven- Thinking correctly under pressure siku moja.
2016-Belgian Federation- Analyse WC14en EC16 siku moja.
2018- University Leuven- Technology in Football siku moja.
Kozi nyingine ni pamoja na Saikolojia, GPS, Hart raye registarationa, uchambuzi wa video pamoja na PPT & Office.


4. ALIPOFANYA KAZI
Levo klabu nchi nafasi kuanza kumaliza
Timu ya taifa Zambia Zambia kocha mkuu 01/7/2018 31/3/2019
Timu ya taifa Cameroon Cameroon msaidizi 01/1/2016 28/2/2018
Levo ya juu OH Leuven Ubelgiji msaidizi 01/1/2015
30/11/ 2015
Levo ya juu Niki Volos Ugiriki kocha wa muda 15/9/2014 31/
10 2014
Levo ya juu Niki Volos Ugiriki msaidizi 01/7/2014
14/9/ 2014
Levo ya kati Fostiras Ugiriki kocha mkuu 12/3 2014 30/6 2014
Levo ya kati Fostiras Ugiriki msaidizi 01/7/ 2013 11/3/2014
Levo ya juu KV Mechelen Ubelgiji kocha mkuu U-20 01/7/2011 30/6/2013


5. MAKOCHA WA NGAZI YA JUU ALIOFANYA NAO KAZI
Broos Hugo ( Cameroon, Club Brugge, RSC Anderlecht na KRC Genk)
Vercauteren Frank – RSC Anderlechnt, KRC Genk, Timu ya taifa ya Ubelgiji, Al Jazira na Samara.
Vergoosen Sef – Rod JC, KRC Genk, Nagoya Grampus Japan na PSV Eindhoven.
Leekens G – Club Brugge, Anderlechnt, timu ya Taifa ya Ubelgiji naTunisia.
Mathijssen Jacky – Club Brugge na Charleroi
Koster Adrie – Ajax, PSV, timu ya Taifa ya Saudi Arabia na Club Africain.


6. WACHEZAJI WAKUBWA ALIOWASAIDIA
Wachezaji ambao aliwasaidia kipindi anafundisha na walifanikiwa ni pamoja
na; Jordy Vanlerberghe (timu ya vijana ya KV Mechelen na Club Brugge),
Xristos Tasoulis (Fostiras kwenda Lens Frankrijk L1), Vincent Aboubakar (toka Valenciennes kwenda FC Porto) Nicolas Kargas (toka Fostiras kwenda Olympiakos. Wengine Frank Boya, Patson Daka, Enock Mwepu.


Kwa CV hii ya kocha mashabiki wa Yanga lazima wakimbie 

Post a Comment

0 Comments