BETI NASI UTAJIRIKE

CEO WA SIMBA AZUNGUMZIA UTAJIRI WA KLABU HIYO

Klabu ya Simba ilifanya mkutano wake wa mwaka 2019 hapo jana huku mambo kadhaa yakijadiliwa kwenye mkutano huo. mtendaji mkuu wa Simba Senzo Mazingisa amewachana wapinzani wa Simba ambao ni Yanga na Azam. Senzo amenukuliwa akisema
"Tupo mahali pazuri ambapo mishahara na posho mbalimbali vinatolewa kwa wakati. Wachezaji wetu wanalipwa vizuri ikilinganishwa na klabu kama Azam na Yanga ambao ni wapinzani wetu wakubwa. Kiwango cha pesa kinachotumika katika usajili na masuala mengine ni kikubwa pia."
.
Haya ni moja kati ya maendeleo muhimu barani Afrika, na klabu chache zinaweza kumudu hatua hii."
.
"Simba ni timu kubwa katika soka la Afrika. Ni jukumu letu sote, hasa kwa wachezaji kufanya vizuri ndani ya uwanja na kuifanya iendelee kutambulika kama klabu kubwa."
.
"Wanachama wakati huu tunafanya mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji, mchakato wa uhakiki wa wanachama wetu, uanzishaji wa matawi wa kibiashara, tuvumiliane na kushirikiana, na tutafanya mchakato huu kwa kasi ya kawaida ili msije kuachwa nyuma."
.
"Usajili wa wachezaji utafanyika kwa namna tofauti. Tutatoa mikataba mirefu kwa wachezaji kwa kuzingatia utaratibu wa kitaalamu, kama unataka kucheza hatua ya nusu fainali ya #CAFCL unahitaji kikosi kitakachoweza kukaa pamoja kwa miaka 3-4. "
.
"Tunahitaji pia kutazama kwa kina muundo wetu wa ukuzaji vipaji kuhakikisha kuwa tunatoa wachezaji wetu wenyewe kama ilivyokuwa hapo awali. Tunahitaji kufuata njia hiyo."


"Tuna mchezo muhimu na watani wa jadi mwezi Januari. Napenda kuwahakikishia kuwa maandalizi na mambo yote ya mchezo huo yapo tayari. Wachezaji watakuwa kambini na tangazo la nani atakuwa kocha mkuu mpya na benchi la ufundi litatoka rasmi Jumatano ijayo."


"Ningependa kuchukua maneno machache kutoka kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, anasema: “Ili kuwepo na maendeleo ya kweli, watu wanapaswa kushirikishwa.” Julius Kambarage Nyerere, kutoka kitabu chake cha Uhuru na Maendeleo mwaka 1973.

Post a Comment

0 Comments